Home news SIMBA:KAZI IPO PALEPALE

SIMBA:KAZI IPO PALEPALE


UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa imani yao kwa msimu wa 2021/22 ni kuweza kufanya vizuri na wataanza kuonyesha ukubwa huo kupitia tamasha la Simba Day linalotarajiwa kufanyika Septemba 19.

Leo ni Wiki ya Simba ambayo inatarajiwa kuwa na matendo ya huruma kwa jamii pamoja na kufanya usafi kabla ya siku ya tamasha yenyewe ambayo ni  Septemba 19, Uwanja wa Mkapa.

Akizungumza na Championi Jumatatu,Kaimu Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema kuwa wapo vizuri kwa ajili ya maandalizi na wanaamini kutakuwa na jambo zuri kwa mashabiki wa timu hiyo.

“Kuna mengi mazuri kwa ajili ya Wanasimba na kazi ipo palepale kutoa burudani pamoja na kuwapa kile ambacho wanastahili mashabiki wetu wa timu hii kubwa.

“Utaratibu na shughuli nyingine zote zinakwenda vizuri timu ikirudi kutoka kambini Arusha kuna mambo mengine yataendelea kutolewa ili waweze kujua hali itakuaje lakini kwa upade wa tiketi hizo zinaendelea kuuzwa,” alisema Kamwaga.

SOMA NA HII  KISA KUACHWA NA SIMBA ...DILUNGA AVUNJA UKIMYA...AFUNGUKA A-Z KUHUSU MKATABA WAKE...'BWALYA' ATIA NENO....

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here