Home Habari za Yanga Leo YANGA YAMUWAHI DIARRA CHAP…KUMPA MKATABA NA MSHAHARA MNONO

YANGA YAMUWAHI DIARRA CHAP…KUMPA MKATABA NA MSHAHARA MNONO

Habari za Yanga SC

YANGA sasa iko mezani na menejimenti ya kipa Djigui Diarra, ili kumuongeza mkataba wa mwaka mmoja ili aendelee kuitumikia, licha ya kuwa amebakiza msimu mmoja kabla ya mkataba wa sasa kumalizika.

Kipa huyo raia wa Mali alisaini mkataba wa miaka mitatu na Yanga unaomalizika mwishoni mwa msimu ujao akiwa na rekodi ya kufanya vizuri katika michuano ya ndani na ile ya kimataifa.

Akiiwezesha Yanga kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita na msimu uliomalizika ilifika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa baada ya kupita zaidi ya miaka 20.

Djigui Diarra amekuwa ni mlinda mlango bora sana kwa misimu yote miwili aliyotua Soka la Bongo, lakini pia mafanikio aliyoonesha hata kwa upande wa Timu ya taifa ya Mali kwa kuisaidia timu hiyo kwenye mashindano ya AFCON huko Ivory Coast.

Msimu uliomalizika Djigui Diarra amefanikiwa kumaliza Ligi akiwa moja wa Makipa bora sana, akiwa na Cleansheet 17 nyuma ya mlinda mlango wa Coastal Union Matampi.

Yanga SC inaelezwa kwamba tayari stahiki za mchezaji uyo wamekamilisha ikiwemo mshahara wake, huku wakitarajia kumupngeza mkataba mpya wa mwaka mmoja.

Injinia Hersi amekuwa ni nguzo uhimu kwa usajili klabu ya Yanga, ambapo ameweza kuwabakiza wachezaji muhimu wa timu hiyo ikiwemo Aziz Ki aliyekuwa akihusishwa kuondoka klabuni hapo.

SOMA NA HII  NI YANGA TENA....TFF WAIKAMUA MAMILIONI YA SHILINGI...ISHU NZIMA IKO NAMNA HIVI AISEE...