Home Habari za Simba Leo BAADA YA KUMUACHA CHAMA..SIMBA YAJIBU MAPIGO KWA MCHEZAJI WA YANGA.

BAADA YA KUMUACHA CHAMA..SIMBA YAJIBU MAPIGO KWA MCHEZAJI WA YANGA.

habari za simba, chama

HABARI ZA KUAMINIKA, kutoka Upande wa Simba ni kwamba  tayri kila kitu kimekamilika na muda wowote Simba wanaweza kutoa Thank You ya mchezaji wake Clatous Chama.

Mabosi wa Simba akiwemo tajiri Mohammed Dewji wamfikia  makubaliano  ya kumuacha mchezaji huyo akatafute changamoto mpya.

Kilichokuwa kinasubiriwa ni Rais wa Heshima wa Simba na Muwekezaji Mo Dewji kuona kama ataweza kutoa dau alilotaka mchezaji huyo ili amwage wino wa kuendelea kukipiga Msimbazi, lakini imekuwa tofauti kwake kwan Tajiri amesema mchezaji huyo aachwe aende anakotaka.

MO Dewji inaelezwa haoni umuhimu wa kuendelea kumbakiza Chama klabuni hapo, kwani umri wake umeenda sana hivyo yeye ameshauri Uongozi huo kutafuta mchezaji mwingine mwenye   umri mdogo ambaye atakuwa na uwezo.

DAU LA CHAMA ALILOTAKA

Clatou Chama mwenye umri wa miaka 33 aliuambia uongozi wa Simba kwamba anataka kiasi cha dola 350,000 na mshahara wa usiopungua dola 15000 ndipo asaini mkataba mpya kwa misimu miwili.

Lakini Uongozi wa Simba ukaona pesa hizo ni nyingi sana hivyo walitaka kumpunguzia lakini akagoma,   baada ya kuendelea kumshawishi ili akubali kusaini hata mwaka mmoja bado mchezaji huyo aliweka ngumu.

Muda wowote Simba itatoa Taarifa kuhusu mchezaji huyo ambaye anapewa nafasi kubwa zaidi ya kujiunga na Yanga, walio tayari kumpa kila anachokitaka.

Yanga wamemuhakikishia Chama kumlipa mshahara wa Mil 47 na dau lake la usjaili zaidi ya Mil 700.

SOMA NA HII  BEKI MPYA WA SIMBA AFUNGUKA KILICHOMSHAWISHI KUJIUNGA NA KLABU HIYO