Home Habari za Yanga Leo YANGA YAHAMIA KWA STRAIKA WA ORLANDO PIRATES…JINA NI HILI

YANGA YAHAMIA KWA STRAIKA WA ORLANDO PIRATES…JINA NI HILI

HABARI ZA YANGA

KLABU ya Yanga SC imeanza kufanya mazungumzo ya kumpata kiungo mshambuliaji Mcongoman, Karim Kimvuidi anayecheza Orlando Pirates ya Afrika Kusini.

Nyota huyo (22), ana uwezo pia wa kucheza winga ya kulia na kushoto hivyo kuwavutia viongozi wa kikosi hicho tangu akikipiga Maritzburg Utd ya Afrika Kusini na DC Motema Pembe.

Ali Kamwe, Afisa Habari wa Yanga amesema kuwa wanatambua kazi kubwa inapaswa kufanyika ili kupata kikosi bora zaidi jambo ambalo linafanyiwa kazi.

“Tutafanya usajili wa kishindo tunatambua kwamba ili kuwa bora ni muhimu kuwa na kikosi imara jambo ambalo linafanyiwa kazi kwa umakini mkubwa.

“Kila kitu kipo kwenye mpango kazi na malengo yetu ni kuona kwamba tunakuwa imara kwa ajili ya msimu mpya mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi tunaamini kwamba kazi itakuwa kubwa.” Alisema Ali Kamwe.

Kwa upande wa Injinia Hersi yeye alisema kwamba msimu huu klabu hiyo  itafanya usajili wenye lengo kuongeza ushindani na makali kwa msimu ujao, huku akiweka wazi kwamba wachezaji muhimu watabaki na kuongezewa mikataba.

Tayari jambo hilo limefanyika, na mfungaji bora wa klabu hiyo na Ligi kuu kwa ujumla Stephen Aziz Ki, ameongezwa mkataba mwingine na bado ataendelea kuwapa furaha sana Yanga.

Huku pia kwa upande mwingine kuna taarifa zinasambaa kwamba, huenda mastaa wawili wa Tanzania kwa sasa wakachez timu moja, ambapo Clatous Chama anapewa nafasi kubwa zaidi ya kucheza na Aziz Ki.

SOMA NA HII  BREAKING NEWS...SIMBA YAMTAMBULISHA KELVIN KIJIRI...ACHUKUA NAFASI YA MWENDA & KAPOMBE