Home Habari za Yanga Leo JEAN BALEKE ANUKIA ZAIDI YANGA…GUEDE APEWA THANK YOU

JEAN BALEKE ANUKIA ZAIDI YANGA…GUEDE APEWA THANK YOU

Habari za Simba

HUENDA Hizi zikawa ni taarifa za kushtukiza kwa mashabiki wa soka nchini, kwamba baada ya Yanga kumbeba Clatous Chama kutoka Simba na Prince Dube aliyekuwa Azam, sasa inafanya mipango ya kumshusha kikosini, Jean Baleke aliyewahi kuwika na Wekundu wa Msimbazi.

Ndio, habari kutoka vyanzo vya kuamnika ni kwamba kwamba kuna uwezekano wa asilimia 99 mshambuliaji huyo aliyeondoka katika dirisha dogo akiifungia Simba mabao manane akawa mali ya Yanga.

Safu ya ushambuliaji ya Yanga inategemewa kuwa na Jean Baleke, Prince Dube, Kennedy Musonda, Sowah na Walidi (Clement) Mzize. Huku viungo wake wakiwa ni Stephan Azizi Ki, Clatous Chota Chama, Pacome ZouaZoua na Max Mpia Nzengeli. Katika hatua nyingine Mabingwa hao wa Nchi wameachana na Joseph Guedde ambaye alikuwa mmoja wa wachezaji waliong’ara msimu uliopita.

Akizngumza kuhusu tetesi za yeye kurudi Bongo, na usajili wake Jean Baleke alisema kwamba kwa upnde wake yupo tayari kucheza katika timu yeyote, iwe Yanga, Azam FC au kama Simba wakimuhitaji arudi tena basi atarudi.

“Tanzania ni nymbani ila bado nina uraia wa Congo DR, Nimerudi hapa kuchukua vitu vyangu, Nasikia watu wanazungumzia kuhusu mimi kucheza Yanga, wengine wanasema njoo Yanga, Njoo Azam, Rudi Simba,timu yeyote ikinipigia niende nanda. Hata Simba wakinipigia simu nirudi nipo tayari kurudi” Jean Baleke

Aidha mchezaji huyo ambaye aliondoka Simba akiwa na mabao 8, amezungumzia juu ya mkataba wake na klabu yake ya sasa Al-Ittihad ya Libya kwamba ulikuwa wa mkopo wa mwaka mmoja, katumikia miezi sita, imebakia sita, hivyo lolote linaweza likatokea.

Jean Baleke ndiye mfungaji bora wa ligi ya Libya, alimaliza na mabao 14, alicheza mechi nane na alifunga hat-trick nne.

SOMA NA HII  AZIZ KI ATUA BONGO KININJA...YANGA YAMFICHA HOTELINI