Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA DABI MWANZA….MWAKALEBELA ASHTUKIA JANJA JANJA YA SIMBA…AIFANYIA UMAFIA WA...

KUELEKEA MECHI YA DABI MWANZA….MWAKALEBELA ASHTUKIA JANJA JANJA YA SIMBA…AIFANYIA UMAFIA WA HATARI…


UMAFIA! Ndivyo utakavyoweza kusema, ni baada ya uongozi wa Yanga kubadili kambi mkoani Mwanza ambako watani wao, Simba watapiga hapo kujiandaa na Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC), maarufu kama Kombe la FA.

Simba na Yanga zinatarajiwa kuvaana Jumamosi hii katika mchezo huo ambao unatarajiwa kupigwa saa kumi kamili jioni kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Timu hizo zote zipo Mwanza kwa ajili ya michezo yao ya mwisho ya Ligi Kuu Bara kabla ya mchezo wa nusu fainali, Simba jana walikuwa CCM Kirumba kuvaana na Geita Gold huku Yanga wenyewe leo Jumatatu watacheza na Biashara Unired katika uwanja huo.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela alisema kuwa timu hiyo, haitaendelea kukaa Mwanza na badala yake kikosi chao kitakwenda Shinyanga kuweka kambi fupi kabla ya nusu fainali.

Mwakalebela alisema kuwa wamefikia maamuzi ya kuhamisha kambi Mwanza baada ya makubaliano ya pande mbili kati ya uongozi na benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu wa timu hiyo, Nasreddine Nabi.

Aliongeza kuwa benchi la ufundi ndio limeomba kubadilishiwa kambi hiyo kwa kutaka kufanya mazoezi kwa kificho kwa hofu ya wapinzani wao Simba kuvamia na kutazama mbinu zao.

 “Tumesikia taarifa za Simba kuendelea kubakia Mwanza mara baada ya mchezo wao wa ligi wa leo (jana) dhidi ya Geita Gold kujiandaa na nusu fainali ya FA ambayo itachezwa CCM Kirumba.

“Hivyo sisi hatutaendelea kukaa hapa na badala yake timu itaelekea Shinyanga mara tu baada ya mchezo wa ligi dhidi ya Biashara.

“Kama unavyofahamu, dabi inapokaribia maandalizi yanatakiwa yafanywe kwa usiri mkubwa, lazima makocha wetu wachague sehemu nzuri watakayofanya maandalizi,” alisema Mwakalebela.

SOMA NA HII  HIVI NDIVYO MKUDE ALIVYOWAUMBUA MAMELOD KWA KUMFUNIKA VIBAYA STAA WA BIL 6....