Home Habari za Simba Leo UKWELI WAFICHUKA SAKATA LA CHAMA…YANGA WAMPA MIL 700…MSHAHARA MNONO

UKWELI WAFICHUKA SAKATA LA CHAMA…YANGA WAMPA MIL 700…MSHAHARA MNONO

Habari za Simba SC

SAKATA la usajili wa fundi Clatous Chama aliyemaliza mkataba wake Simba, limezidi kuchukua sura mpya, baada ya bosi mmoja wa Zambia kuvujisha siri kiungo huyo tayari amesaini mkataba wa mwaka moja Yanga.

Ingawa sio Chama wala Yanga waliothibitisha juu ya dili hili, lakini taarifa za ndani kutoka Yanga ni kiungo huyo atakuwa mali ya kikosi hicho kwa msimu ujao.

Inaelezw kwamba Yanga wamempatikia Chama ofa na mkataba mzuri wa dau la usajili dola 300,000/= (Milioni  785 TZS, huku mshahara wake ukielezwa kuwa ni dola 15,000/= sawa na Mil 39 kwa pesa ya  Kitanzania

Chama na Uongozi wa Simba bado hakijeleweka ambapo msimamo wa Chama anahitaji kupewa dau kubwa la usajili na mshahara wa Tsh Milion 50.

Bosi wa Simba amekataa kutoa pesa kubwa kwa mchezaji huyo ambapo mwanzo walikuwa wanamuomba aongeze angalau mkataba wa mwaka mmoja lakini Chama hajaongeza mkataba hadi muda huu.

Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Yanga zinasema kila kitu kipo tayari na muda wowote kama mambo yakienda sawa, Chama atacheza yanga msimu ujao.

Kwa upande wa Simba mashabiki wengi wameonekkana kuchukuizwa na tabia za mchezaji huyo kuwasumbua kwenye usajili, kwahiyo baadhi yao wanaona ni muda muafaka kwa viongozi wao kuachana na mchezaji huyo.

Inaelezwa kwamba Simba wameingia sokonikutafuta mchezaji atakayekuwa mbadala wa Chama, na tayari wamempata mmoja Joshua Mutale ambaye anaweza kucheza nafassi ya namba 10, winga na kiungo mchezeshaji.

SOMA NA HII  SAKATA LA YANGA LAMFIKIA WAZIRI NDUMBARO...ATETA JAMBO NA INJINIA HERSI.