Home Habari za Simba Leo SIMBA YAHAMISHIA NGUVU KWA KIUNGO…MAGORI ASIMAMIA SHOW NZIMA

SIMBA YAHAMISHIA NGUVU KWA KIUNGO…MAGORI ASIMAMIA SHOW NZIMA

HABARI ZA SIMBA

FAGIO la chuma limeendelea kupitishwa katika klabu ya Simba, mabosi wa klabu hiyo wapo bize kuingiza majembe mapya, kwani baada ya beki Lameck Lawi, tayari imemvuta kiungo mwingine fundi kutoka Mashujaa.

Simba imemsajili kiungo huyo, Omary Omary ikielezwa kashapewa mkataba wa miaka miwili na kilichobaki ni kutangazwa kama ilivyokuwa kwa Lameck Lawi aliyenyakuliwa kutoka Coastal Union iliyoamua kuikataa biashara hiyo na Wekundu hao, ingawa inaelezwa kitasa hicho kitacheza.

Omary ni moja kati ya wachezaji wa ndani walioonesha kiwango kizuri sana akiwa na Mashujaa, ambapo aliisaidia timu hiyo kusalia kwenye Ligi Kuu ya NBC, huku mambo yake na Simba yakiwa sehemu nzuri zaidi.

Uongozi wa Klabu ya Simba umendelea kufanya sajili nyingi ili kutengeneza timu itakayokuwa na makali ambayo yalipotea kwa misimu mitatu nyuma.

Simba hadi sasa wamekamilisha sajili nyingi huku wakiendelea kutafuta wachezaji wengine ambao watakuwa na kikosi tishio kwa misimu ijayo.

Sajili ambazo zinasubiri kutambulishwa hadi sasa ni, Elie Mpanzu, Joshua Mutale, Yusuph Kagoma, Kelvin Kapumbu, Serge Pokou na wengine sajili zao zinaendelea ikiwemo Antony Tra Bi Tra na wengine ambao bado majina yao yanaendelea kufanyiwa kazi.

Crescentius Magori ni moja ya kiongozi anayesimamia usajili  wa Klabu ya Simba, na inaelezwa kishaanza kazi  mapema sana, huku   akitembelea nchi kama Zambia kusaka wachezaji.

SOMA NA HII  KUHUSU SIMBA KUFIKA FAINAL YA CAF...ZIMBWE Jr AWAPIGA 'BREKI' WANAOWAZA HIVYO...ATAJA HATUA HIZI..