Home Habari za michezo KIULAINIII….NABI AFUNGA MACHO NA KUSAINI MKATABA MPYA YANGA….AKATAA MAMILIONI YA WAARABU…

KIULAINIII….NABI AFUNGA MACHO NA KUSAINI MKATABA MPYA YANGA….AKATAA MAMILIONI YA WAARABU…


Klabu ya Soka ya Yanga imethibitisha kocha wake Nasredin Mohammed Nabi ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuwatumikia timu hiyo ya ‘Wananchi’ hadi mwaka 2024.

Licha ya Nabi kuhitaji ongezo zaidi la mshahara ambao wameafikiana, kingine ni mipango yake ndani ya mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania.

Kila Kocha anapenda kufanikiwa na timu anayofundisha hata kama haipendi. Nabi anaamini anaweza kupata mafanikio aliyokosa alikopita, kama Yanga wanavyoamini pia juu yake hasa kufuatia kuimarishwa kwa kila idara ndani ya kikosi hicho msimu huu.

Nabi ameiongoza Yanga kutwaa mataji matatu mhimu msimu uliyopita baada ya Yanga kuwa na ukame wa makombe kwa miaka minne.

Baada ya kusaini kandarasi hiyo, Nabi amesema; “Bado nipo nipo sana, Safi fresh.”

SOMA NA HII  INJINIA HERSI AMWAGA HADHARANI SIRI ZA JINSI YANGA WATAKAVYOBEBA UBINGWA KIUULAINIII...