Home Uncategorized DILUNGA AYAKUMBUKA MABAO YAKE

DILUNGA AYAKUMBUKA MABAO YAKE


HASSAN Dilunga, kiungo mshambuliaji wa Simba amesema kuwa ameikumbuka Ligi Kuu Bara ikiwa ni pamoja na yale mabao yake aliyofunga akiwa ndani ya uwanja.
Dilunga amefunga mabao sita ndani ya ligi ambayo ilisimamishwa Machi 17 kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona.
Dilunga amesema kuwa:”Nimekumbuka mpira kwa sasa na kuona namna ambavyo tunaendelea kufanya vizuri kwani kwa sasa hakuna ambacho kinaendelea nina amini ligi ikirejea mambo yatakuwa sawa.”
Mechi ya kwanza ya Hassan Dilunga ndani ya Simba aliyojiunga nayo msimu wa 2018/19 akitokea Mtibwa Sugar ilikuwa dhidi ya Tanzania Prisons, Agosti 22 Uwanja wa Taifa na Simba ilishinda bao 1-0.

Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kurejea Juni Mosi baada ya Serikali kuruhusu shughuli za michezo ambazo zilisimamishwa Machi 17 kutokana na janga la Corona.
SOMA NA HII  KOCHA ARSENAL AWASIFU WACHEZAJI WAKE ASEMA HAWAJAMUANGUSHA