Home Habari za michezo KABLA KIZA HAKIJAWA KIKALI LEO…SIMBA KUSHUSHA KIFAA KINGINE CHA KAZI …NI STRAIKA...

KABLA KIZA HAKIJAWA KIKALI LEO…SIMBA KUSHUSHA KIFAA KINGINE CHA KAZI …NI STRAIKA LA MAGOLI HASWA…


Kama ulikuwa unadhani wamemaliza jua unajiongopea, Wekundu wa Msimbazi Simba SC, leo Agosti 5, 2022 wanashusha jembe jipya la kazi katika safu ya ushambuliaji.

Hayo yamezungumzwa mapema hii leo na Msemaji wao, Ahmed Ally alipokuwa akifanya mahojiano na kituo cha radio cha Wasafi alipokuwa akizungumzia tamasha lao la Simba Day ambalo linatarajia kuchukua nafasi Agosti 8, 2022.

“Tunatarajia kutangaza mchezaji mwingine mpya hii leo ambaye atakuwa ni mshambuliaji,” alisema Ahmed.

Msemaji huyo alisema, baada ya kuachana na wachezaji watatu jana, Kagere, Wawa na Lwanga, wanazo nafasi mbili za kujaza idadi ya wachezaji wa kigeni ambapo moja wapo ndio hiyo wanayokwenda kuijaza.

Amesema, baada ya hapo wataangalia tena kama wanaweza kuongeza mchezaji mwingine wa kigeni au la.

Aidha, msemaji huyo alimzungumzia kiungo wao Kanuti ambaye hakuonekana na kikosi nchini Misri ambapo alisema alikuwa anashughulikia masuala yake ya Paspoti na sasa tayari yupo nchini na leo anatarajia kujiunga na wenzake kuendelea na mazoezi kwa ajili ya msimu ujao.

SOMA NA HII  RALLY BWALYA - YANGA WALIZIDIWA NA SIMBA KWENYE KUNISAJILI KWA SABABU HII..!!