Home Uncategorized KAHATA WA SIMBA AMECHEMSHA

KAHATA WA SIMBA AMECHEMSHA


Kocha wa Kenya, Sebastian Migne amekiri kwamba staa mpya wa Simba, Francis Kahata hakuwa na bahati kwenye Afcon ya msimu huu.

Migne amekiri kwamba hata kwenye mechi na Tanzania hakuwa na wakati mzuri ingawa inawezekana alipania sana. Hata kwenye mechi na Algeria mchezaji huyo alitolewa mapema baada ya kushindwa kuhimili mchezo.

Kocha huyo anasema kwamba Kahata ni miongoni mwa mastaa ambao aliwapa nafasi kubwa ya kutisha msimu huu lakini ikawa tofauti ingawa hamlaumu kwa vile soka ndivyo ilivyo na Afcon ni mashindano makubwa.

Kahata ameripotiwa kusaini mkataba na Simba akiwa nchini hapa na atakuwa akilipwa Sh 8 mil kwa mwezi.

SOMA NA HII  KIKOSI CHA AZAM FC KITAKACHOANZA LEO UWANJA WA TAIFA DHIDI YA SIMBA