Home Uncategorized MBWANA SAMATTA BWANA! KUMBE KITAMBO TU ANAPAMBANA

MBWANA SAMATTA BWANA! KUMBE KITAMBO TU ANAPAMBANA


MBWANA Samatta anayekipiga Aston Villa kwa sasa mechi yake ya kwanza kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ilikuwa Machi 20, 2011dhidi ya TP Mazembe.

Zama hizo alikuwa anakipiga Simba iliyokuwa inafundishwa na Patrick Phiri.

2015 akiwa TP Mazembe, Desemba 13 alicheza mechi yake ya kwanza kwenye Kombe la Dunia la Klabu na walichapwa mabao 3-0.

Mkononi ana tuzo ya mchezaji bora wa Afrika aliyoipata mwaka 2015 pia aliingia kwenye kikosi bora cha CAF mwaka 2015 pamoja na tuzo ya mfungaji Bora wa Ligi ya Afrika usisahau na kiatu cha Ebony hiyo ilikuwa 2019.


Alipotua Genk, Samatta alipewa jezi namba 77 ila alipokichafua sana alipewa jezi namba 10 ambayo ndiyo aliyokuwa anaivaa ndani ya timu ya Taifa ya Tanzania.

Kwa sasa akiwa na Aston Villa ameanza na jezi namba 20 akifanya maajabu tena mambo yatakuwa mswano kwake.


Mechi yake ya kwanza ilikuwa kwenye Kombe la Carabao dhidi ya Leicester City na timu yake ilishinda mabao 2-1 na imetinga fainali itamenyana na Manchester City.

Mchezo wake wa kwanza kwenye Ligi Kuu England alitupia bao lake la kwanza.

SOMA NA HII  SAFARI YA MWISHO YA ALIYEKUWA OFIA HABARI WA SIMBA ASHA MUHAJI IMEHITIMISHWA LEO