Home Uncategorized LICHA YA KUCHIMBISHWA SPURS, MUARGENTINA POCHENTINO ANA REKODI TAMU KWELI

LICHA YA KUCHIMBISHWA SPURS, MUARGENTINA POCHENTINO ANA REKODI TAMU KWELI

LICHA ya Mauricio Pochentino kupigwa chini ndani ya Tottenham Hotspurs baada ya kudumu kwa miaka mitano na nafasi yake kuchukuliwa na Jose Mourinho bado Muargentina huyo ana rekodi tamu.

Pochentino alichimbishwa na wasaidizi wake ambao ni Jesus Perez aliyekuwa kocha msaidizi na makocha wengine Miguel d’ Agostino na Antoni Jimenez kutokana na timu hiyo kuwa na mwenendo mbovu.

Wakati huo Spurs ilikuwa nafasi ya 14 kwenye msimamo ilishinda mechi tatu pekee kati ya 12 na kujikusanyia pointi 14 kibindoni kwa sasa ipo nafasi ya sita ikiwa na pointi 37 imecheza jumla ya mechi 25.

Pochentino tangu atue Spurs 2014 aliisaidia timu hiyo kumaliza ndani ya nafasi nne kwenye Ligi Kuu England mara nne kabla ya hapo timu ilimaliza kwenye nafasi hiyo mara mbili misimu 22 iliyopita.

Pia Pochentino alifanikisha timu hiyo kushiriki fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo ilichapwa na Liverpool.

Msimu wa 2014/15 aliibuka mshindi wa pili wa Kombe la Ligi na alisaini dili la miaka mitano Mei 2016 ila upepo ukambadilikia fasta.

Kwa sasa inaelezwa kuwa ana matumaini ya kuwa Kocha Mkuu ndani ya Manchester United.

SOMA NA HII  TUIPE SAPOTI TIMU YETU YA TAIFA TUWEKE KANDO TOFAUTI ZETU