Home Ligi Kuu WANAUME 22 LEO KAZINI KUSAKA POINTI TATU

WANAUME 22 LEO KAZINI KUSAKA POINTI TATU



LEO Mei 11, Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea ambapo kutakuwa na mchezo mmoja kwa wanaume 22 kusaka pointi tatu muhimu.

Mwadui FC ya Shinyanga itawakaribisha ndugu zao Kagera Sugar, Uwanja wa Mwadui Complex.

Mchezo wa leo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na nafasi ambazo timu hizo zipo kwenye hatari ya kushuka daraja.

Mwadui FC kwenye msimamo ipo nafasi ya 18 ikiwa na pointi 19 baada ya kucheza jumla ya mechi 28 huku Kagera Sugar ikiwa nafasi ya 17 na ina pointi 27 baada ya kucheza jumla ya mechi 28.

SOMA NA HII  BREAKING: MAPILATO WA SIMBA V YANGA HAWA HAPA