Home news KOCHA MKUU WA SIMBA ASHTUKA JAMBO,ABADILI GIA KWA MTINDO HUU

KOCHA MKUU WA SIMBA ASHTUKA JAMBO,ABADILI GIA KWA MTINDO HUU


 WAKATI kikosi chake kikionekana bado hakina muunganiko mzuri, Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes, ameamua kuwarudisha fasta mazoezini nyota wake kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana.

Gomes amelazimika kukirejesha kikosi chake mazoezini baada ya kuwa na mapumziko ya siku mbili tayari kwa kujiandaa na mchezo huo wa hatua ya kwanza utakaochezwa Oktoba 14, mwaka huu nchini Botswana.

Taarifa kutoka ndani ya Simba, zimeliambia Spoti Xtra kwamba, Gomes bado hajaridhishwa na kiwango cha kikosi chake, hivyo amewataka mastaa wote ambao hawajaenda kwenye timu zao za taifa kuwasili mazoezini bila kukosa ili aweze kuwanoa kabla ya kukutana na Wabotswana hao.

“Kocha amesema kuwa tayari amewafuatilia wapinzani wetu wale Wabotswana na kuona uchezaji wao, hivyo hawezi kutoa siku za mapumziko zaidi ya mbili kwa wachezaji wake, pamoja na kwamba hawajapata muda mrefu wa kupumzika.

“Sababu kubwa ni kwamba bado haridhishwi na muunganiko wa kikosi chake na angependa kutumia muda huu kuweka sawa muunganiko huo,” kilisema chanzo hicho.

Tayari wachezaji wa Simba ambao hawajaitwa kwenye timu zao za taifa wameanza mazoezi ikiwa ni pamoja na Ibrahim Ajibu, Jonas Mkude, Beno Kakolanya, Pascal Wawa.

SOMA NA HII  BENCHIKHA AFURAHIA JAMBO JIPYA SIMBA....