Home Simba SC KISA WACHEZAJI WAPYA…GOMES AVUNJA UKIMYA MSIMBAZI…AMTAJA CHAMA NA MIQUISSONE

KISA WACHEZAJI WAPYA…GOMES AVUNJA UKIMYA MSIMBAZI…AMTAJA CHAMA NA MIQUISSONE


Wiki kadhaa tangu kutimka Clatous Chama na Luis Miquissone kwenye kikosi cha Simba, kocha Didier Gomes amevunja ukimya akiainisha namna alivyoziba mapengo ya wachezaji hao.

Chama na Miquissone waliondoka Simba wakati huu wa usajili wa dirisha kubwa, kipindi ambacho bado mashabiki wa Simba walikuwa wakiwahitaji.

Jana, Gomes kwa mara ya kwanza alizungumzia kuwakosa nyota hao ambao walikuwa ni chaguo lake la kwanza kwenye kikosi cha Simba.

“Lengo ni kuwa na kikosi imara hata baada ya kuondoka kwa Luis na Chama,” alisema kocha Gomes jana kutoka kambini nchini Morocco.

Msimu huu, timu hiyo imewasajili wazawa sita na wageni watano ambao ni Hennock Inonga ‘Varane’, Peter Banda, Duncan Nyoni, Sadio Kanoute na Pape Sakho kutoka nje na Israel Patrick, Kibu Denis, Jimmyson Mwanuke, Abdulsamad Kassim, Jeremiah Kisubi na Yusuph Mhilu.

Akizungumzia mwenendo wa kambi yao nchini Morocco inayokaribia wiki ya tatu sasa kwenye mji wa Rabat kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao, kambi ambayo kocha Gomes alisema inampa matokeo bora.

“Nimeanza kupata kombinesheni ya timu kwa kipindi ambacho tumekuwa kambini nchini hapa, japo changamoto ambayo nipo nayo sasa ni idadi ya wachezaji kupungua na wengi kwenda kwenye timu za taifa,” alisema Gomes.

Chama na Miquessone kwa pamoja walihusika katika mabao 40 ya Simba msimu uliopita, wakati nyota hao wakifunga na kutoa pasi za mabao zilizosaidia miamba hiyo kutwaa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara nne mfululizo.

Chama alifunga mabao nane huku akitoa pasi za mabao 13, wakati Miquessone akiweka mpira wavuni mara tisa, huku pasi zake 10 zikizaa mabao kwenye Ligi Kuu.

Wachezaji zaidi ya 10 wa timu hiyo wameitwa kweye timu zao za Taifa, miongoni mwao ni Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Mohammed Hussein na John Bocco ambao wameitwa Taifa Stars.

Simba ambayo katika kambi ya Morocco itacheza mechi tatu za kirafiki na moja walitarajiwa kucheza jana jioni baada ya ile ya awali na FAR Rabat, ambayo ni ya jeshi nchini humo iliyomalizika kwa sare ya mabao 2-2, imesalia na wachezaji 18 kambini.

SOMA NA HII  MORRISON NA MKASA WA MTENGENEZA DUBWANA...ALISAJILIWA SIMBA KIMAFYA NA BADO AKAIFUNGA AKIWA YANGA...

“Hii ni changamoto ambayo inanisumbua hapa kambini, wachezaji wengi wamekwenda kwenye timu zao za taifa, lakini kwa kipindi tulichokuwa wote huku, tulipambana kutengeneza kombinesheni na kufanikiwa,’ alisema.

Alisema hadi kufikia kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya watani zao, Yanga atakuwa ameamilisha kazi kwa asilimia 95 kwenye kikosi chake.