Home Uncategorized JKT TANZANIA V SIMBA MATOKEO YAO YA MECHI ZAO HAYA HAPA

JKT TANZANIA V SIMBA MATOKEO YAO YA MECHI ZAO HAYA HAPA

 


LEO Uwanja wa Jamhuri, Dodoma saa 10:00 jioni utachezwa mchezo kati ya JKT Tanzania dhidi ya Simba.

Ikiwa ni mzunguko wa tano kwa sasa tayari timu zote mbili zimecheza mechi zao nne ndani ya ligi.

Rekodi zinaonyesha kuwa JKT Tanzania imeshinda mechi moja nyumbani kwa ushindi wa bao moja kwa bila huku ikishinda mechi moja ugenini mbele ya Kagera Sugar.

Imepoteza mchezo mmoja nyumbani mbele ya Dodoma FC kwa kufungwa bao moja na imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Polisi Tanzania ugenini.

Imefunga jumla ya mabao mawili na kufungwa mabao matatu.

Matokeo yake yalikuwa namna hii:-Kagera Sugar 0- 1 JKT Tanzania, Uwanja wa Kaitaba.

JKT Tanzania 0-1 Dodoma Jiji FC, Uwanja wa Jamhuri.

Polisi Tanzania 1-1 JKT Tanzania, Uwanja wa Ushirika Moshi.

Coastal Union 1-0 JKT Tanzania, Uwanja wa Mkwakwani.


Kwa upande wa Simba yenyewe imecheza mechi nne pia imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 mbele ya Mtibwa Sugar, imeshinda tatu moja ilikuwa ugenini dhidi ya Ihefu kwa mabao 2-1 na zile mbili za nyumbani ilishinda ilikuwa mbele ya Biashara United kwa mabao 4-0 na mbele ya Gwambina kwa mabao 3-0.


Ilikuwa namna hivi matokeo yake:-

Ihefu 1-2 Simba, Uwanja wa Sokoine.


Mtibwa Sugar 1-1 Simba, Uwanja wa Jamhuri, Moro.


Simba 4-0 Biashara United, Uwanja wa Mkapa.

Simba 3-0 Gwambina Uwanja wa Mkapa.


Kwenye mechi nne imefunga mabao 10 na imefungwa mabao mawili.

SOMA NA HII  SABABU ZA MORRISON KUSHIKILIWA NA POLISI DAR HII HAPA