Home Uncategorized TOWNSHIP ROLLERS WATUA NA MAJI YAO DAR KUCHEZA NA YANGA TAIFA –...

TOWNSHIP ROLLERS WATUA NA MAJI YAO DAR KUCHEZA NA YANGA TAIFA – VIDEO


KUEPUKA kufanyiwa hujuma na wapinzani wao Yanga, kikosi cha Township Rollers, jana kilitua jijini Dar es Salaam kikiwa na vinywaji vyao ikiwemo maji na juisi. Township walitua jana jioni wakiwa na msafara wa watu 38 wakiwemo benchi la ufundi, makocha na baadhi ya viongozi wa timu hiyo.

Kikosi hicho kitacheza na Yanga, kesho Jumamosi katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo itachezwa kwenye Uwanja wa Taifa kuanzia saa 12 jioni. 

Championi Ijumaa, ambalo ndiyo gazeti pekee lililokuwepo wakati kikosi hicho kikitua nchini kiliwahushudia baadhi ya wachezaji hao wakisukuma matoroli ambayo yalikuwa na vitu mbalimbali.

 Kikosi hicho kilitua jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius 
Nyerere (JNIA). Wametua Bongo wakitokea Afrika Kusini ambapo walipitia baada ya kutoka kwao Botswana

SOMA NA HII  VPL:SIMBA 0-0 JKT TANZANIA