Home Habari za michezo NEEMA ZAZIDI KUMIMINIKA YANGA….WASAINI MKATABA WA KUIPA KLABU MABILIONI YA PESA KAMA...

NEEMA ZAZIDI KUMIMINIKA YANGA….WASAINI MKATABA WA KUIPA KLABU MABILIONI YA PESA KAMA SIMBA….KAZI NDIO INAANZA…

 


Klabu ya Yanga imeandika historia nyingine mpa leo Ijumaa, Agosti 19, 2022 baada ya kuingia makubaliano na kusaini mkataba wa miaka miwili wa kufanya kazi na kampuni iliyobobea katika masoko ambayo ni ya wazawa iitwayo Jackson Group.

Akizungumza kabla ya kusaini mkataba huo, Rais wa Klabu ya Yanga, Mhandisi Hersi Said amesema baada ya kufanya mabadiliko ya Katiba na kuruhusu umiliki wa hisa asilimia 51 kwa Wanachama na asilimia 49 kwa wawekezaji, klabu hiyo sasa imefungua milango kwa wawekezaji kuja kuwekeza na kufanya biashara na Yanga.

“Kabla ya kuingia madarakani, moja ya ajenda yangu moja ya mambo ambayo niliahidi wakati wa kampeni ni kuifanya Yanga iwe kibiashara ili iingize pesa. Yanga ndiyo klabu kongwe hapa Tanzania na ndiyo klabu yenye mataji mengi na wanachama wengi, lakini ukubwa na thamani yake hauendani na maendeleo yake.

“Hivyo tumeona badala ya kuajiri Mkurugenzi wa Masoko tukamlipa pesa, ni bora kutafuta kampuni ambayo ina uzoefu mkubwa kwenye masuala ya masoko, ili watuletee wawekezaji na kutushauri mbinu bora za klabu kufanya biashara na kuingiza pesa, klabu itaingiza pesa na itakuwa rahisi hata kujenga uwanja kama nilivyoahidi.

“Hatutaweza kujenga uwanja ama kupata maendeleo makubwa kama klabu kama hatuna mipango endelevu ya kiuchumi na yenye tija. Hivyo tunawakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara kuja kuwekeza Yanga,” amesema Hersi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Jackson Group, Kelvin Twisa amesema wameamua kuingia makubaliano hayo na Yanga baada ya kuona kwamba ndiyo klabu bora Tanzania na yenye uongozi unaojielewa, wataweza kusimamia vyema haki za mdhamini.

“Tuna uzoefu mkubwa katika masuala ya biashara za mpira, nimesimamia mikataba ya Vodacom na Bodi ya Ligi wakati huo nikiwa Vodacom, tumefanya biashara na Simba, Yanga, Gor Mahia ya Kenya na Ligi Kuu ya Kenya. Pia, klabu za La Liga, na Arsenal na Hull City za Uingereza, hivyo tunafahamu vizuri biashara ya mpira inavyofanyika, sasa kazi yetu ni kwenda kuiuza Yanga na kuitafutia masoko.

SOMA NA HII  WAARABU WAPANGA VIINGILIO 'BABU KUBWA' MECHI YAO NA YANGA...TIKETI ZINAUZWA LAKI...

“Tuna uhakika kwa hiki tunachokwenda kukifanya na Yanga, klabu itapata pesa na thamani yake sambamba na wawekezaji kukuza biashara zao na kupata kile wanachokitarajia. Yanga ni kubwa, ina viongozi makini, ndiyo maana imekuwa rahisi kwetu kufanya nao kazi, tunawakaribisha wawekezaji tuje kufanya kazi,” amesema Twisa.