Home Habari za michezo WAARABU WAPANGA VIINGILIO ‘BABU KUBWA’ MECHI YAO NA YANGA…TIKETI ZINAUZWA LAKI…

WAARABU WAPANGA VIINGILIO ‘BABU KUBWA’ MECHI YAO NA YANGA…TIKETI ZINAUZWA LAKI…

Habari za Yanga

Kuelekea Mechi ya Kombe la Ligi ya Mabingwa Barani Afrika baina ya Al Merrikh dhidi ya Young Africans Sports Viingilio vimewekwa wazi.

Gharama ya kuangalia mchezo huo katika Uwanja wa Pele nchini Rwanda ni Tsh 104,391 (50K Franc), tsh 52,195 (25K Franc) na cha chini kabisa ni shilingi 20,870 (10K Franc).

Al Merrikh watakuwa wenye katika ardhi ya Rwanda Uwanja wa Pele, dhidi ya Young Africans Sports majira ya saa 10:00 Alasiri.

MUSONDA ‘AWACHOCHA’ WAARABU..

Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Mzambia, Kennedy Musonda amesema kuwa yeye na wachezaji wenzake wapo fiti na tayari kuwavaa wapinzani wao Al Merrikh ya nchini Sudan.

Timu hizo zinatarajiwa kuvaana Jumamosi (Septemba 16) kwenye Uwanja wa Kigali Pele ulio katika Mji wa Kigali, Rwanda ambako utapigwa mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Musonda amesema kuwa maandalizi aliyoyafanya yanatosha kuwapa furaha mashabiki wa timu hiyo, kuelekea mchezo dhidi ya Al Merrikh.

Musonda amesema kuwa wanahitaji ushindi dhidi ya Al Merrikh watakaokuwa nyumbani ili kuwaongezea presha wapinzani wao, watakaporudiana jini Dar.

“Kama mchezaji nipo tayari na fiti asilimia mia moja kucheza mchezo dhidi ya Al Merrikh, ni mchezo ambao tunahitaji kupata ushindi kwa lengo la kuwapa furaha mashabiki wetu.

“Kikubwa nilichopanga ni kutumia vema kila nafasi nitakayokuwa ninaipata katika mchezo huo kwa kufunga mabao na kuwatengenezea wachezaji wenzangu. “Ninaamini mchezo utakuwa mgumu, lakini nitahakikisha ninaipambania timu yangu, kama nikipata nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza,” amesema Musonda.

SOMA NA HII  BAADA YA KUCHEZA JUZI..KIWANGO CHA SAIDO CHAMFANYA NABI AGUNE...AMVUNJIA UKIMYA..AMWELEZA HAYA....