Home news BAADA YA KUCHEZA JUZI..KIWANGO CHA SAIDO CHAMFANYA NABI AGUNE…AMVUNJIA UKIMYA..AMWELEZA HAYA….

BAADA YA KUCHEZA JUZI..KIWANGO CHA SAIDO CHAMFANYA NABI AGUNE…AMVUNJIA UKIMYA..AMWELEZA HAYA….

 


BAADA ya kiungo mshambuliaji wa Yanga, Said Ntibazonkiza ‘Saido’ kucheza mechi yake ya kwanza msimu huu ndani ya Ligi Kuu Bara, kocha mkuu wa timu hiyo, Nasreddine Nabi ameonekana kuvutiwa na uwezo wake.

Juzi Jumanne, Saido alicheza mechi dhidi ya Ruvu Shooting iliyochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar ambpo aliingia kipindi cha kwanza akitokea benchi kuchukua nafasi ya Yacouba Songne aliyeumia.

Akizungumza na Gazeti la Spoti Xtra, Kocha Nabi alisema: “Ntibazonkiza alicheza vizuri, ni mchezaji mkubwa na kila mtu anafahamu hilo, ndani ya Yanga kila mtu anayo nafasi ya kucheza kama ambavyo wengine hucheza.“

Siwezi kusema kwa kuhakikisha atacheza katika michezo ijayo, lakini nafasi ni nzuri kwake kutokana na alichokionesha leo (juzi).”

SOMA NA HII  BAADA YA MASHABIKI WA SIMBA KULIA KWAMBA 'WANAOUMIA NI WAO'...TRY AGAIN AIBUKA NA KUWAJIBU HIVI.....