Home Habari za michezo BAADA YA KUSHUSHIWA MASHINE YA KAZI…GAMONDI AANZA UPYAA YANGA…

BAADA YA KUSHUSHIWA MASHINE YA KAZI…GAMONDI AANZA UPYAA YANGA…

Habari za Yanga leo

KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema ameongeza dozi ya mazoezi kwa kuwafanyika mazoezi wachezaji wake mara mbili kwa siku, ili wale watakaorudi kutoka AFCON wawakute wako fiti.

Kocha huyo amesema kwa jinsi alivyoona michuano ya AFCON ni kwamba wachezaji wote wa timu yake ambao wapo huko na vikosi vya vya taifa wanaongeza vitu vingi ikiwemo ufundi, pumzi na fiziki, hivyo anataka na waliobaki nao wasikae bure au kufanya mazoezi mepesi kwani hawatokuja kuwa sawa.

Kikosi cha Yanga kinaendelea kufanya mazoezi mara mbili kwa siku jioni uwanja wa Avic Town uliopo Kigamboni Dar es Salaam na asubuhi mazoezi ya Gym ili kujiweka wachezaji wake kuwa katika utimamu wa mwili.

Gamondi amesema kipindi cha Ligi Kuu Tanzania Bara imesimama kuendelea kwa fainali za AFCON, lakini timu yake haitakuwa na muda wa kupumzika kwa sababu wanatambua wanakibarua kigumu mbele yao ikiwemo mchezo wa ligi na kimataifa.

Amesema baada ya mapumziko mafupi walipotoka katika michuano ya Mapinduzi na sasa wamerejea na kutengeneza timu yao ikiwemo kutengeneza muunganiko wa nyota wapya ambao wamesajiliwa kipindi cha dirisha dogo.

“Tunaendelea na mipango yetu kwa sababu bado kazi kubwa ipo mbele yetu na ukiangalia wachezaji baadhi walikuwa kwenye mapumziko mafupi hawakuwepo katika Kombe la Mapinduzi tumerejea mapema kuweza kujipanga kwa muda huu wachezaji wapya wameingia wanahitaji kuzoea timu ili tufikie malengo,” amesema Gamondi.

Ameongeza kuwa anahitaji wachezaji wake wote kuwa vizuri kwa sababu wanamichezo mingumu mbele yao ikiwemo ligi ambao watachexa dhidi ya JKT Tanzania kabla kukutana na CR Belouizdad ya Algeria.

Ameeleza kuwa usajili umefanywa kulingana na mahitaji yake kwa kufanyia kazi na kuongeza baadhi ya wachezaji ambao wataenda kuimarisha katika kila eneo ikiwemo sa

SOMA NA HII  ROBERTINHO AFUNGUKA ULIPO UDHAIFU WA SIMBA