Home Habari za michezo KAMA ULIKUWA HUJUI…UBABE WOTEE WA YANGA KWA SIMBA UKO KWA NABI…TIRIRIKA NA...

KAMA ULIKUWA HUJUI…UBABE WOTEE WA YANGA KWA SIMBA UKO KWA NABI…TIRIRIKA NA TAKWIMU HIZI A-Z….


Achana na ubabe wa kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi dhidi ya Simba ambapo katika mechi saba za mashindano tofauti walizokutana, ameshinda mara nne, kutoka sare mbili na kupoteza mechi moja.

Rekodi hiyo imemfanya Nabi awe kocha wa Yanga aliyeifunga Simba mara nyingi zaidi ndani ya muda mfupi kuliko mwingine yeyote tangu ilipoanzishwa mwaka 1935.

Kocha huyo amedhihirisha umwamba mwingine kwa kuiongoza Yanga kufikia rekodi ya Azam FC ya kucheza mechi 38 mfululizo za Ligi Kuu bila kupoteza baada ya timu yake kupata ushindi wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Polisi Tanzania juzi.

Lakini tofauti na Azam ambayo wakati inaweka rekodi ya kutopoteza mechi 38 ilikuwa chini ya makocha wawili tofauti, Nabi amefikia rekodi hiyo akiiongoza Yanga akiwa pekee ambapo mara ya mwisho kupoteza ilikuwa ni dhidi ya Azam Aprili 25, 2021 walipofungwa bao 1-0.

Wakati Azam inacheza mechi 38 bila kupoteza, ilianza kunolewa na Stewart Hall ambaye nafasi yake ilichukuliwa na Joseph Omog. Hall aliiongoza Azam kucheza michezo 21 bila kupoteza kabla ya kutimuliwa Novemba, 2013 ambapo nafasi yake ilichukuliwa na Omog ambaye chini yake, Azam ilicheza mechi 13 za Ligi Kuu bila kupoteza hadi Oktoba 25, 2014 walipofungwa bao 1-0 nyumbani na JKT Ruvu ambayo sasa ni JKT Tanzania.

Katika mechi 38 ambazo Nabi ameiongoza Yanga kwenye Ligi Kuu bila kupoteza, timu hiyo imeibuka na ushindi michezo 28 na sare 10. 

Ukiondoa rekodi hiyo, Nabi ameiongoza Yanga kuimarisha rekodi ya kuwa timu iliyocheza idadi kubwa ya mechi mfululizo za ugenini za Ligi Kuu bila kupoteza.

Yanga imecheza michezo 21 mfululizo ugenini Ligi Kuu bila kupoteza, idadi ya mechi nne zaidi ya rekodi iliyoshikiliwa na Simba na Azam.

Simba na Azam zilikuwa zikishikilia rekodi ya kucheza michezo mingi mfululizo Ligi Kuu ugenini bila kupoteza ambapo kila moja ilicheza mechi 17 nyakati tofauti.

Kitendo cha kutoka nyuma dhidi ya Polisi Tanzania na kuibuka na ushindi (come back) kumeifanya Yanga itimize mechi ya nane ya mashindano chini ya kocha Nabi kufanya hivyo.

SOMA NA HII  "NITAKA JEZI YA MANULA...PALE SIMBA NAMBA YANGU IKO ...."

Kabla ya juzi, Yanga ilitoka nyuma baada ya kutanguliwa na kuibuka na ushindi dhidi ya Simba, Geita Gold, Tanzania Prisons, Biashara United, Azam na Coastal Union, Ruvu Shooting.

Akizungumzia rekodi za Nabi, mchezaji wa zamani wa Yanga, Makumbi Juma ‘Homa ya Jiji’ alisema zinadhihirisha ubora wa kocha huyo.

“Ukiangalia Yanga imekuwa ikiimarika siku hadi siku na Nabi anafanya vizuri katika kuimarisha viwango vya wachezaji, jambo ambalo limekuwa likiisaidia timu kufanya vizuri,” alisema.