Home Habari za michezo HAYA HAYA….MNIGERIA HUYU KUMRITHI AKPAN SIMBA….MAMBO YAPELEKWA MCHAKA MCHAKA KUIWAHI CAF….

HAYA HAYA….MNIGERIA HUYU KUMRITHI AKPAN SIMBA….MAMBO YAPELEKWA MCHAKA MCHAKA KUIWAHI CAF….


Kiundo wa Simba, Victor Akpan huenda akatolewa kwa mkopo kutokana na kushindwa kumshawishi kocha, Zoran Maki ili kumpatia nafasi ya kucheza katika michezo mitatu iliyocheza timu hiyo hadi sasa.

Akpan alisajiliwa na Simba kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Coastal Union baada ya kuonyesha kiwango bora msimu uliopita kwenye Ligi Kuu Bara pamoja na kombe la Shirikisho (ASFC).

Akpan anacheza nafasi ya kiungo mkabaji ambayo kwenye mechi dhidi ya St George, Yanga na Geita Gold walitumika, Jonas Mkude, Sadio Kanoute na Mzamiru Yassin ambao wawili hawa hawakuwa kwenye pre-season kule Misri.

Inaelezwa kutokana na Akpan kushindwa kumshawishi, Zoran huenda akarudishwa kwa mkopo Coastal Union na nafasi yake ikachukuliwa na kiungo mpya kutokea Kwara United FC kutokea Ligi Kuu ya Nigeria, Afeez Nosiru.

Mabosi wa Simba inaelezwa wameanza mchakato wa kutafuta kiungo mpya wa ukabaji na Nosiru anapewa nafasi kama chaguo la kwanza ingawa kuna chaguo la pili kama kiungo wa zamani wa Kaizer Chiefs, Teddy Akumu.

SOMA NA HII  SIMBA YAMUWEKA KANDO BEKI HUYU AMBAYE WANATAJWA KUIWINDA SAINI YAKE