Home Uncategorized UWANJA WA TAIFA KUWA NA MASHABIKI ELFU 30 SIMBA V YANGA

UWANJA WA TAIFA KUWA NA MASHABIKI ELFU 30 SIMBA V YANGA


MASHABIKI watakaoruhusiwa kuutazama mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya nusu fainali, Julai 12 ni 30,000.

Simba itakuwa uwanjani ikimenyana na Yanga kwenye mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Sababu ya kufanya hivyo ni kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.

Serikali ilitoa agizo kwamba kwenye mechi zenye uwezo wa kuchukua mashabiki wengi lazima mashabiki waingie uwanjani nusu kwa kuwa Uwanja wa Taifa una uwezo wa kuchukua mashabiki 60,000 basi nusu yake ni 30,000.

Mashabiki pia wanapaswa wafuate kanuni za afya ambazo zimekuwa zikitolewa mara kwa mara juu ya kujikinga na Corona.

Taratibu hizo ni pamoja na kuvaa barakoa wakati wa kwenda uwanjani, kunawa mikono kwa maji tiririka na kukaa umbali wa mita moja.


SOMA NA HII  BARAKA THE PRINCE ATAJA SABABU ZA KUFUTA PICHA ZA MPENZI WAKE - VIDEO