Home Uncategorized NYOTA MWINGINE, MTAMBO WA MABAO NDANI YA YANGA HATIHATI KUIKOSA SIMBA JULAI...

NYOTA MWINGINE, MTAMBO WA MABAO NDANI YA YANGA HATIHATI KUIKOSA SIMBA JULAI 12


JUMA Abdul nahodha wa Yanga yupo kwenye hatihati ya kuwakosa wapinzani wao Simba kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Julai 12.


Kwa sasa Abdul mzawa ambaye ni kinara wa pasi za mabao ndani ya Yanga akiwa nazo sita anasumbuliwa na jeraha la kifundo Cha mguu wa kushoto alilopata kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United.

Mchezo huo ulichezwa Julai 5, Uwanja wa Karume na dakika 90 zilikamilika kwa sare ya bila kufugana.

Abdul alikosekana katika mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Julai 8 wakati Yanga ikishinda bao 1-0.


Daktari wa Yanga, Shecky Mngazija alisema kuwa bado wanaendelea kumfanyia matibabu kwa sasa ili awe fiti hivyo wataangalia hali yake itakavyokuwa kesho.

SOMA NA HII  RUVU SHOOTING HAWAAMINI WANACHOKIONA TPL