Ratiba hiyo imewekwa wazi huku baadhi ya timu zikiwa na viporo vya hatua ya 16 bora hii ni kutokana na michuano hiyo kusimama kutokana na janga la Virusi vya Corona ambalo liliivurugavuruga dunia.
Barcelona mchezo wake wa awali ilitoa sare ya 1-1 na Napoli na sasa itacheza Agosti pale Camp Nou na ikishinda itakutana na Bayern Munich. Man City wao waliifunga Real Madrid 2-1 pale Santiago Bernabeu na sasa watakuwa Etihad na atakaye shinda kati ya Juventus na Lyon ambapo Juve alipoteza kwa bao 1-0.
Klabu ambazo ratiba yao ipo moja kwa moja ni pamoja na RB Leipzig atavaana na Atletico Madrid ambao waliwang’oa mabingwa watetezi Liverpool.
Atalanta wabishi wa Serie A wao wataavana na mabingwa wa Ligue 1 Paris Saint German ambapo katika hatua hiyo ya nusu fainali zitachezwa mechi nne zikishirikisha timu nane.
Michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itaanza kupigwa mwezi ujao na itafanyika nchini Ureno katika jiji la Lisbon awali ilikuwa ifanyike Instanbul.
1. Madrid / Man City vs Lyon / Juventus
2. RB Leipzig vs Atletico Madrid
3. Napoli / Barcelona vs Chelsea /Bayern Munich
4. Atalanta vs Paris Saint-Germain
Kwa upande wa Europa League ambayo imefika hatua ya robo fainali kwa upande wake michezo ya hatua ya 16 mechi zake zote hazikukamilika.
Hivyo kwa Europa ratiba yao itakuwa hivi mshindi kati ya Shakhtar Donesk v Wolfburg atacheza na Basel au Frankfurt, Man United v LASK mshindi atacheza na Copenhgen au Instanbul Basaksehir.
Inter v Getafe watacheza na mshindi kati ya Leverkusen au Rangers, huku mshindi kati ya Wolves v Olympiacos atacheza na Roma au Sevilla na fainali ya michuano hii itachezwa Ujerumani.