Home Uncategorized BAADA YA KUANZA KWA KUCHECHEMEA, COASTAL UNION YAZINDUKA

BAADA YA KUANZA KWA KUCHECHEMEA, COASTAL UNION YAZINDUKA


Jana Julai 9, timu ya Coastal Union ilisepa na pointi tatu Uwanja wa Sokoine kwa ushindi wa mabao 2-1.

Mabao yote kwa Coastal Union yalijazwa kimiani na Shaban Idd Hamisi.

 Coastal Union baada ya ligi kuendelea pale ilipoishia haikuwa na mwendo mzuri ambapo ilifungwa jumla ya mabao saba na kufunga mabao matatu kwenye mechi zake tano zilizopita.

Ilianza Juni 13, Coastal Union 2-2 Namungo FC, Uwanja wa Mkwakwani, Juni 20,Coastal Union 0-0 Mtibwa Sugar,Uwanja wa Mkwakwani, Juni 23, Mbao FC 1-0 Coastal Union, Uwanja wa CCM Kirumba.


Juni 27, Alliance 1-0 Coastal Union, Uwanja wa Kirumba na ilimaliza kupokea kichapo Julai 6, Mbeya City 3-1 Coastal Union, Uwanja wa Sokoine kabla ya jana kusepa na pointi tatu.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA