Home Uncategorized SIMBA WAIVUTIA PUMZI UD SONGO, MAKALI YAO YOTE KWA AZAM FC

SIMBA WAIVUTIA PUMZI UD SONGO, MAKALI YAO YOTE KWA AZAM FC


PATRICK Aussems, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa hesabu kubwa ni mchezo wake wa ngao ya jamii dhidi ya Azam FC utakaopigwa Jumamosi uwanja wa Samora, Iringa.

Aussems amesema mpango wa mechi ya kimataifa dhidi ya UD do Songo ameuweka kando kwa muda. 


“Hesabu kubwa ni kuona tunapata matokeo kwenye mchezo wetu dhidi ya Azam ambao utaanza kabla ya marudiano na UD do Songo.

 “Nikimaliza kucheza na Azam nitakuwa na muda wa kuifikiria UD do Songo na nina amini utakuwa mchezo mgumu na wenye ushindani,” amesema.

Mchezo wa kwanza wa kimataifa hatua ya awali Simba ililazimisha sare dhidi ya UD Songo ya Msumbiji hivyo wana kazi kupata matokeo mechi ya marudiano ili kusonga mbele inayotarajiwa kuchezwa kati ya Agosti 23-25.

SOMA NA HII  RATIBA YA FAINALI YA LIGI YA KUKAPU TANZANIA LEO HII HAPA