Home Habari za michezo MEYA DAR:- SIMBA HATUNA KOCHA….YANGA WALITUZIDI KILA KITU….

MEYA DAR:- SIMBA HATUNA KOCHA….YANGA WALITUZIDI KILA KITU….

Habari za Simba

Aliekuwa Meya wa Manispaa ya Ubungo ambae pia ni shabiki kindaki ndaki Klabu ya Simba, Boniface Jacob ameeleza kile alichokiona katima mchezo wa Fainali ya Ngao ya Jamii kati yao na Yanga SC.

Mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa CCM Mkwakwani juzi Jumapili, Agosti 13, 2023 na kumalizika kwa sare ya bila kufungana, Simba iliibuka mshindi kwa changamoto ya mikwaju ya penati 3-1.

Katika mchezo huo, Yanga walionekana kuwa bora zaidi kuliko Simba kuanzia kipindi cha kwanza ambapo mpaka mwisho wa mchezo

Boniface Jacob ameyaandika haya; “Simba hatuna kocha, tunasajili halafu tunaogopa kutumia wachezaji wazuri, tunaweka walewale tukitegemea matokea mapya, mtani alituzidi kimbinu na kiuwezo ndani ya Uwanja, Yanga haijabomoka kama tulivyotegemea (labda kama walikamia), hahati ni yetu,” amesema Boniface Jacob.

SOMA NA HII  WAKATI TAARIFA ZA 'VIJIWENI' ZIKISEMA KOCHA SIMBA ANAWACHUKIA CHAMA NA PHIRI...KUMBE UKWELI WA MAMBO UKO HIVI...

1 COMMENT