Home news EHE…ILE ISHU YA STRAIKA WA MBEYA CITY, KIBU DENIS KUJIUNGA SIMBA IKO...

EHE…ILE ISHU YA STRAIKA WA MBEYA CITY, KIBU DENIS KUJIUNGA SIMBA IKO HIVI KUMBE….


IMEISHA hiyooo! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mabosi wa Simba kumalizana na mshambuliaji nyota, Kibu Denis na kupanga kumtambulisha mara timu itakaporejea nchini kutoka Rabar Morocco ilipoenda kupiga kambi ya maandalizi ya msimu mpya.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Simba, msafara wa mwisho wa Simba utarudi nchini Septemba 4 na timu huenda ikaenda kupiga kambi ya kujiandaa na mechi yao ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga, mjini Karatu, lakini wakiwa humo watafanya utambulisho wa Kibu waliyemng’oa Mbeya City.

Kibu pamoja na kipa Jeremiah Kisubi walishindwa kuambatana na timu Morocco, pia kutotambulishwa kama wenzao kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao, lakini taarifa zinasema kwa sasa kila kitu kipo sawa na majembe hayo yawasubiri wenzao kwenda kambini Karabu katika Kituo cha Black Rhino.

Imeelezwa suala lililochelewesha utambulisho wa Kibu na wenzake kwa sasa limeisha na jamaa wanasubiri kundi la pili lirudi kutoka Morocco na kuungana na wale waliopo timu za taifa ili kumalizia maandalizi yao kabla ya kuvaana na Yanga Septemba 25.

Wachezaji waliopo timu za taifa ni Perfect Chikwenda (Zimbabwe) Taddeo Lwanga (Uganda) Meddie Kagere (Rwanda) na wengine nane waliopo Taifa Stars ambao ni Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein, Erasto Nyoni, Mzamiru Yassin, Israel Mwenda, Kennedy Juma na John Bocco.

SOMA NA HII  BAADA YA KUSIKIA YANGA WANAMTAKA....KAZADI AWATUPIA MPIRA SINGIDA BIG STARS....