Home Yanga SC IMEFICHUKA..MASTAA WOTE WAPYA WA YANGA KUKOSEKANA KESHO..SABABU HIZI HAPA

IMEFICHUKA..MASTAA WOTE WAPYA WA YANGA KUKOSEKANA KESHO..SABABU HIZI HAPA

KIUNGO wa Yanga, Mukoko Tonombe atakosekana kesho Jumapili katika Kilele cha Wiki ya Mwananchi.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alisema kuwa nyota huyo atakosekana kwa sababu ya majukumu ya timu ya Taifa.

“Mukoko anaondoka alfajiri kuelekea Congo kwenye majukumu ya timu ya Taifa hivyo ni mchezaji pekee atakayekosekana kesho,” alisema.

Katika hatua nyingine Mwakalebela amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi ili kutoa sapoti katika kikosi hicho kinachotarajiwa kucheza na Zanaco ya Zambia.

“Nawasihi mashabiki wa Mwanza, Mbeya, Iringa, Dodoma na kwingineko kujitokeza kwa wingi ili kujionea tamasha kubwa la kihistoria, “alisema.

DR Congo itakutana na Tanzania Septemba 2, katika mchezo wa kufuzu kombe la Dunia nchini Qatar Mwaka 2022.

Mbali na Mukoko nyota wengine ambao watakosekana ni Khalid Aucho, Yanic Bangala ambaye atasafiri na Tonombe, kipa Diarra ambaye amefiwa na baba yake.

SOMA NA HII  GAMONDI- AL MERRIKH WANAPIGIKA KIRAHISI TU...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here