Home Uncategorized COASTAL UNION: TUMEADHIBIWA KWA MAKOSA YETU WENYEWE

COASTAL UNION: TUMEADHIBIWA KWA MAKOSA YETU WENYEWE


 BAADA ya kugawana pointi mojamoja na wapinzani wake Gwambina kwenye sare ya kufungana bao 1-1 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Kocha Mkuu wa Coastal Union, Juma Mgunda amesema kuwa waliadhibiwa kutokana na makosa ambayo waliyafanya.


Kwenye mchezo huo wa ligi uliochezwa jana, Oktoba 24, Coastal Union ilianza kufunga kupitia kwa Yusuph Soka dakika ya pili bao hilo lilipinduliwa na Meshack Abraham kinara wa utupiaji ndani ya Gwambina akiwa na mabao manne dakika ya 36.


Mgunda amesema kuwa wachezaji walishindwa kulinda ushindi wao na kufanya makosa ambayo pia yalisababisha wawape penalti Gwambina, Yusuph Dunia dakika ya 15 alikosa penalti hiyo wakati timu yake bado ikiwa nyuma kwa bao 1-0.


Mgunda amesema:-“Tumefanya makosa wenyewe na ndio maana tumeadhibiwa, tulianza kushinda mapema tukashindwa kulinda ulinzi wetu hivyo tumepata ambacho tulistahili kupata hapa nyumbani.


“Nampongeza mwalimu mwenzangu kwa kuwa tumesoma naye hivyo  tulikuwa tunapambana huku tunajuana sio mbaya, makosa ambayo wachezaji wameyafanya ninayachukua na tunakwenda kufanyia kazi.”


Coastal Union kwenye msimamo ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi tisa baada ya kucheza mechi nane ndani ya Ligi Kuu Bara wa msimu wa 2020/21.

SOMA NA HII  MOURINHO:NILIWAHESHIMU WAPINZANI