Home Habari za michezo KUELEKEA MSIMU UJAO….YANGA NI FULL KICHEKO…SIMBA WATAMBA KUTAWALA TENA CAF…

KUELEKEA MSIMU UJAO….YANGA NI FULL KICHEKO…SIMBA WATAMBA KUTAWALA TENA CAF…


Ni zamu ya mashabiki wa Yanga kutamba kila kona, kutokana na timu hiyo kubakiza mechi moja tu kutangaza ubingwa msimu huu.

Yanga inaongoza kileleni kwa pointi 64, ikishinda mchezo mmoja kati ya minne iliyobakia itafikisha pointi 68 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote, kwani mtani wake wa jadi Simba ana 51 na akishinda mechi tano zilizobakia itafikisha 66.

Uhakika wa ubingwa huo kwa Yanga, umemfanya shabiki kindakindaki wa timu hiyo anayetambulika kwa jina la  Anwari Mwita Wambura ‘Yanga Kigelegele’ kujimwambafai.

“Mtaani tunasikika Yanga tu wenzetu  wapo wapi? wamepoa kama vile wamehama nchini, jamani jamani Yanga ni tamu hii,” amesema Yanga Kigelege na ameongeza;

“Mchezo huu hauhitaji makasiriko, raha ya kigelegele ukikipiga angalau uitikiwe na majirani zako, hii ndio Yanga ya mataji bhana.

Shabiki mwingine anayejulikana kama Jesca Manji, amesema ni mwaka wa rangi za kijani na njano kutamba kila kona, huku akiwataka majirani zao (Simba) wapumzike.

“Sikuona timu ya kuizuia Yanga kunyakua mataji ya Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho Azam (ASFC), ina kikosi kizuri, huu ni mwaka wa wetu wa kutamba,”amesema.

Justin Joel  ambaye ni shabiki wa Simba lialia na mtendaji mkuu wa tawi la Wekundu wa Msimbazi, amejibu mapigo akiwaambia watani wao, wakutane kimataifa. “Tukutane michuano ya CAF ambako kutaonyesha ukomavu wa kila timu na uzuri hatujabebwa na timu yoyote kucheza michuano hiyo kwa mwaka huu, hivyo  Wanasimba hatuna sababu ya kutembea kinyonge,” amesema.

SOMA NA HII  KISA UCHEZAJI WA YANGA KWENYE LIGI...SENZO AIBUKA NA HILI..AMTAJA GOLIKIPA DIARRA