Home Habari za michezo GAMONDI AGEUKA KIVURUGE KWA WAPINZANI

GAMONDI AGEUKA KIVURUGE KWA WAPINZANI

MIGUEL Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga, amevuruga ramani za wapinzani wake wanaofikiria mbinu yake ya kupata mabao itakuwa kwa washambuliaji pekee wanaonza kikosi cha kwanza ikiwa ni Clement Mzize na Kenedy Musonda.

Mrithi huyo wa mikoba ya Nasreddine Nabi, ameibuka na mbinu mpya kwenye upande wa ushambuliaji tofauti na Nabi ambaye alikuwa akimtumia zaidi Fiston Mayele eneo la utupiaji misimu miwili mfululizo.

Akizungumza na Spoti Xtra, Gamondi alisema kuwa kinachofanyika kwa sasa ni timu nzima kutafuta matokeo ya ushindi bila kujali nani ambaye atapata nafasi ya kufunga kwenye mchezo husika.

“Ikiwa utakuwa unawategemea washambuliaji peke yake inakuwa rahisi kwa wapinzani kutuzuia na mwisho wa siku wachezaji wangu watakwama kutupa ushindi, hivyo wanacheza wakiwa ni timu.

“Kila mchezaji anafunga awe ni beki, kiungo na hata washambuliaji nao wanafunga jambo ambalo ni zuri kwetu. Makosa tunayafanyia kazi ili kuwa imara kwa wakati ujao kwa kuwa mechi ni nyingi na ushindani ni mkubwa,” alisema Gamondi.

SOMA NA HII  SIMBA NA YANGA ZAFANYA KUFURU...ZIMEVUNA MAMILIONI HAYA KWA DK 90 TU