Home Uncategorized MBEYA CITY: HALI NI MBAYA KWETU

MBEYA CITY: HALI NI MBAYA KWETU

KOCHA Msaidizi wa Mbeya City,Mohamed Kijuso amesema kuwa timu yake ipo kwenye hali mbaya msimu huu kutokana na matokeo mabovu ambayo wanayapata jambo linalowafanya wapambane kupata matokeo.

Mbeya City jana iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Lipuli kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Kijuso amesema:”Wote mnatambua kwamba kwa sasa mwenendo wa Mbeya City sio mzuri, hali ni mbaya kutokana na matokeo tunayoyapata tunachokifanya kwa sasa ni kupambana kurejea kwenye ubora wetu na kupata matokeo mazuri.

“Mashabiki waendelee kutupa sapoti kwani nafasi ya kufanya vizuri ipo na kila kitu kinawezekana,”. 

Mbeya City ipo nafasi ya 18 ikiwa na pointi 21 huku Lipuli ikiwa nafasi ya 12 na pointi zake 29.

SOMA NA HII  ILIKUWA KITAMBO, SAINI YA NAHODHA WA MTIBWA SUGAR NA SASA NI KOCHA MKUU, CHEKI MAFANIKIO YAKE