Home Uncategorized MTIBWA SUGAR YAPATA PAKUTOKEA LEO

MTIBWA SUGAR YAPATA PAKUTOKEA LEO

UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa leo utapambana kupata matokeo mbele ya Tanzania Prisons kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Mtibwa Sugar haijapata ushindi kwenye mechi zake ilizocheza mwezi Februari ina kumbukumu ya kuchapwa bao 1-0 na JKT Tanzania kwenye mchezo wake uliopita.

Thobias Kifaru, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar amesema kuwa watapambana kupata matokeo mazuri ili kurejea kwenye ubora wao.

“Hatujawa na matokeo mazuti kwa sasa hilo lipo wazi ila matokeo mabaya yanatuumiza nasi pia tunapambana kuona namna gani tutarejea kwenye ubora wetu mashabiki waendelee kutupa sapoti.

“Kwenye mchezo wetu dhidi ya Prisons tutapambana kupata ushindi jambo litakaloturudisha kwenye ubora wetu,” amesema.

Prisons ililazimisha sare ya bila kufungana na Yanga Uwanja wa Taifa ipo chini ya Adolf Rishard.

SOMA NA HII  YANGA IPO KAMILI GADO KUIVAA TANZANIA PRISONS