Home Uncategorized SIMBA YATAJA SABABU YA KUSHINDWA KUFUNGA MABAO MENGI MBELE YA KAGERA SUGAR

SIMBA YATAJA SABABU YA KUSHINDWA KUFUNGA MABAO MENGI MBELE YA KAGERA SUGAR

NAHODHA wa Simba, John Bocco amesema kuwa wapinzani wao Kagera Sugar walicheza kwa kiwango bora jambo lililowafanya washindwe kuwafunga mabao mengi kutokana na nafasi walizotengeneza.

Bocco aliongoza kikosi chake cha Simba jana, Februari 18 Uwanja wa Taifa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar lililofungwa na Meddie Kagere kwa mkwaju wa penalti uliosababishwa na Bocco mwenyewe dakika ya 60.

“Kagera Sugar walicheza vizuri na ilikuwa chanzo kwetu kushindwa kufunga mabao mengi, ni kitu kizuri kukutana na ushindani nasi tunajipanga kwa ajili ya mechi nyingine.

“Kwa matokeo ambayo tumeyapata ya ushindi tunamshukuru Mungu na kuwaa pongez wapinzani wetu,  kushinda kwetu tunafurahi kwani ni furaha kwetu na mashabiki pia,” amesema.

Bocco amefunga mabao matatu ndani ya ligi na ana pasi moja ya bao pia amesababisha penalti moja iliyofungwa na Kagere baada ya kuchezewa rafu na Benedick Tinnoco ndani ya 18.

SOMA NA HII  SAMATTA AANZA KAZI KWENYE MAKAZI YAKE MAPYA