Home Uncategorized SAMATTA AANZA KAZI KWENYE MAKAZI YAKE MAPYA

SAMATTA AANZA KAZI KWENYE MAKAZI YAKE MAPYA


NYOTA wa Tanzania, Mbwana Samatta muda mfupi baada ya kuibukia ndani ya Klabu ya Fenerbahce ya Uturuki kwa mkopo akitokea Klabu ya Aston Villa ameanza kupiga matizi na wachezaji wenzake ndai ya kikosi chake kipya.

Samatta ameandika rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Ligi Kuu England na kufunga bao pia baada ya kuibukia huko akitokea Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji.

Alisaini dili la miaka minne ndani ya Astov Villa ambayo iliponea chupuchupu kushuka daraja kwa msimu wa 2019/20.


Klabu ya Aston Villa imemuaga nyota huyo kupitia ukurasa wao wa Instagram kwa inamtakia kila la kheri kwenye maisha yake mapya.


Mchezaji huyo aliyeshinda taji la mfungaji bora mara kadhaa nchini Ubelgiji kabla ya kujiunga na Aston Villa nchini Uingereza atahudumu katika klabu hiyo kwa mkopo wa mwaka mmoja kabla ya kuandikisha kandarasi ya kudumu ya miaka minne.


Samatta amesema kuwa anafurahia maisha yake mapya na anawashukuru Aston Villa kwa kumpa nafasi ya kucheza kwenye ligi ya ndoto yake.

SOMA NA HII  HAWA HAPA NYOTA WANNE WA YANGA KUJUA KAMA PANGA LITAWAHUSU WIKI HII