Home news NAMUNGO YAPANIA KUFANYA VIZURI KIMATAIFA

NAMUNGO YAPANIA KUFANYA VIZURI KIMATAIFA


 HEMED Morocco, Kocha Mkuu wa timu ya Namungo FC amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya 1 de Agosto unaotarajiwa kuchezwa Februari 14, nchini Angola.

Kikosi cha Namungo FC leo kimewafuata wapinzani wao kikiwa na nyota wao 22 huku nyota wake Adam Salamba akibaki kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Morocco amesema kuwa wanatambua kwamba Watanzania wanapenda matokeo mazuri jambo ambalo linawapa nguvu ya kwenda kupambana.

“Tunajua kwamba Watanzania wanahitaji matokeo mazuri nasi pia tupo tayari kwa ajili ya ushindani kikubwa mashabiki waendelee kutuombea dua.

“Kila timu inahitaji ushindi hilo lipo wazi nasi pia tunahitaji kupata matokeo chanya hivyo yale makosa ambayo tuliyafanya kwenye mechi zetu zilizopita tutayafanyia kazi,” .

SOMA NA HII  RASMI....SIMBA WATOA TAMKO HILI ISHU YA INONGA KUTAKIWA NA FAR RABAT YA NABI...