Home Habari za michezo RASMI….SIMBA WATOA TAMKO HILI ISHU YA INONGA KUTAKIWA NA FAR RABAT YA...

RASMI….SIMBA WATOA TAMKO HILI ISHU YA INONGA KUTAKIWA NA FAR RABAT YA NABI…

Habari za Simba leo

UONGOZI wa Simba umefunguka kuhusu kile kinachoeleza juu ya beki wao Enock Inonga kuwindwa na aliyekuwa kocha wa zamani wa Yanga, Nasreddine Nabi anayekinoa kikosi cha AS FAR Rabat ya Morocco.

Nabi ameutaka uongozi wa timu ya AS Far Rabat kuhakikisha wanaipata saini ya beki kisiki wa Simba, Inonga kwa lengo la kukuiongozea nguvu kikosi chake kinachoshiriki Ligi Kuu ya nchini hiyo maarufu kama Botola Liegue.

Nabi ambaye msimu uliopita amejiunga na timu hiyo baada ya kumaliza mkataba wake na Yanga ameipa mafanikio ya kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita katika mchezo waliopoteza kwa bao la ugenini dhidi ya MC Alger.

Taarifa za uhakika kutoka kwa vyanzo ya kuaminika vinaeleza kuwa Nabi amependekeza kusajiliwa beki huyo ambaye yupo katika michuano ya mataifa Afrika Afcon na timu yake ya Taifa ya DR Congo ilifuzu hatua ya 16 bora kwenye michuano hiyo.

Licha ya Nabi kusisitiza kumtaka beki huyo mwenye thamani ya Dola laki tano ambayo sawa na shilingi bilioni 1.2 ambaye amebakisha mkataba wa mwaka mmoja ndani ya timu hiyo.

“Nabi amewaambia mabosi wa timu yake kuhakikisha wanaipata saini ya beki wa Simba, Inonga Kwa ajili ya maboresho ya kikosi chake ingawa wanatambua hali halisi ya thamani ya mchezaji wenyewe ambaye bado anamkataba na Simba unaotarajia kufikia ukingoni mwakani”, amesema mtoa taarifa.

Lakini alivyotafutwa ofisa habari wa Simba, Ahmed Ally amesema hawezi kuongea jambo lolote kwa kuwa bado hajapokea ofa yoyote mezani inamuhusisha beki huyo.

“Sisi Kwa sasa hatuna jambo lolote la kusema kama ni kweli au vipi Kwa sababu uongozi bado hauna ofa yoyote inamuhusisha Inonga na klabu yoyote zaidi tunaendelea na maandalizi ya Ligi,” amesema Ahmed.

Ameongeza kuwa nyota huyo mkataba wake unamalizika mwakani na ikatokea ofa hiyo imefika kwenye meza yao hilo suala la kumuuaza au kuendelea naye itakuwa katika mapendekezo kati ya benchi la ufundi linaloongozwa na Abdelhak Benchikha na uongozi.

SOMA NA HII  ACHANA NA SAIDOO...CHUMA HIKI KINGINE CHA MAANA KUTUA SIMBA SC...MBRAZILI KAMPITISHA..

1 COMMENT