Home Uncategorized ILIKUWA KITAMBO, SAINI YA NAHODHA WA MTIBWA SUGAR NA SASA NI KOCHA...

ILIKUWA KITAMBO, SAINI YA NAHODHA WA MTIBWA SUGAR NA SASA NI KOCHA MKUU, CHEKI MAFANIKIO YAKE

KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zubery Katwila mkataba wake wa kwanza kusaini ilikuwa ni mwaka 1999 mbele ya mmoja wa wakurugenzi wa wakati huo Mr. Bube.

Katwila alikuwa kwenye wakati mzuri alipojiunga na Mtibwa Sugar kwani mwaka huo wa 1999 timu yake ilitwaa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara na ilitetea pia taji hilo mwaka 2000 kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru.

Pia Katwila akiwa ni nahodha alikiongoza kikosi hicho kutwaa Kombe la Mapinduzi mwaka 2000 na alikuja kukiongoza tena kikosi hicho kutwaa Kombe la Mapinduzi mwaka 2020 kwa kuitungua Simba bao 1-0.

Katwila amesema:”Nakumbuka nilitwaa taji la Mapinduzi nikiwa nahodha mwaka 2000, ilikuwa ni wakati mzuri kwetu na timu kiujumla,”.

SOMA NA HII  SINGIDA UNITED YA MINZIRO YASAKA WACHEZAJI 10 KATI YA 500