Home Habari za michezo MWAMUZI AFUNGUKA UTATA WA PENATI ZILIZOOKOLEWA NA ALLY SALIM DHIDI YA YANGA...

MWAMUZI AFUNGUKA UTATA WA PENATI ZILIZOOKOLEWA NA ALLY SALIM DHIDI YA YANGA JUZI…

Habari za Simba

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi, Salum Umande Chama, amevunja ukimya kutokana na utata uliojitokeza baada ya mchezo wa Ngao ya Jami, kati ya Young Africans dhidi ya Simba SC.

Utata ulioibuka ni namna Mlinda Lango wa Simba SC, Ally Salim alivyokuwa akiokoa mikwaju iliyopigwa na wachezaji wa Young Africans ambapo alifanikiwa kuzuia Penati tatu za Khalid Aucho, Pacome Zouzoua na Yao Attohoula.

Katika mchezo huo wa fainali ya Ngao ya Jamii uliochezwa juzi Jumapili (Agosti 13) kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Simba SC iliibuka na ushindi wa Penati 3-1 dhidi ya Young Africans, baada ya muda wa kawaida matokeo kuwa 0-0.

Baada ya kumalizika kwa mchezo huo, wadau mbalimbali wa soka wamekuwa wakihoji wakidai kwamba, waamuzi waliruhusu Ally Salim kutoka kwenye mstari kabla ya pigo la Penati.

Mbali na hilo, pia mwamuzi wa kati, Jonesia Rukyaa, alilalamikiwa kwa namna ya uamuzi wake ambapo wapo waliosema aliegemea upande mmoja, huku maamuzi yake mengi yakiwa si sahihi.

Bosi huyo wa zamani wa waamuzi ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Kagera, amesenma tangu mwanzo hadi mwisho wa mchezo huo, hakukuwa na chembe yoyote ya upendeleo iliyofanywa na waamuzi, huku akibainisha kwamba, kulikuwa na dosari ndogo ambazo hazikuathiri chochote.

“Kwa ujumla dosari zilikuwa ndogo ambazo wala hazikuleta athari zozote za mchezo.”

Kuhusu madai ya Ally Salim kutoka kwenye mstari kabla ya pigo la Penati, Umande amesema: “Siyo rahisi hilo kulizungumzia, ndiyo maana wenzetu Ulaya wana VAR ambayo huonesha vitu kama hivyo.

“Pigo la Penati wakati linapigwa, si rahisi kuona makosa madogo kama hayo, sasa hao wanaozungumzia hilo jambo utagundua wamefanya hivyo baada ya mchezo kuisha, walikaa na kutafakari, lakini mchezo unapokuwa unaendelea sio rahisi sana kutambua kitu kama hicho hasa kwa mwamuzi. Mimi ninaona mchezo umechezeshwa vizuri, mambo yote yameenda ‘fair’.

SOMA NA HII  PAMOJA NA MASIFAA YOOTE ANAYOPEWA....MAYELE ATUMIA DAKIKA 1,161 KUFUNGA GOLI SABA TU...