Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA KESHO YA CAF….GAMONDI AFUNGUKA ATAKAVYOIMALIZA KAZI MAPEMA…

KUELEKEA MECHI YA KESHO YA CAF….GAMONDI AFUNGUKA ATAKAVYOIMALIZA KAZI MAPEMA…

Habari za Yanga SC

MWAKILISHI wa Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga inashuka dimbani kesho kusaka ushindi wa pili kwenye mchezo wa marudiano ya Michuano hiyo dhidi ya AS Al Sabieh (Asas FC) kutoka Djibouti.

Huo unakuwa mchezo wa pili baada ya mechi ya pili kushinda bao 2-0 katika mechi hiyo ambayo ulipigwa katika uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi na leo wanarudiana dhidi ya Asas FC katika dimba hilo na Yanga wakiwa nyumbani.

Yanga wanahitaji kushinda kwenye mchezo wa kesho ili kusonga mbele kwenye Ligi hiyo ya Mabingwa Afrika, akivuka hatua hiyo atakutana na mshindi mchezo wa El Mareikh ya Sudan dhidi ya Otoho FC ya Congo Brazilian.

Kikosi cha Yanga kinanolewa na Kocha Miguel Angel Gamondi ambaye anahitaji kuona timu yake ikicheza soka nzuri na kupata ushindi mkubwa kwa kila mechi watakayocheza.

Kuelekea mechi ya kesho, Gamondi alisema baada ya ushindi wa mechi ya kwanza wanafuata matokeo hayo na kuanza 0-0 kwa sababu anahitaji kuona timu yake inacheza mpira mzuri.

Alisema hakufurahishwa kwa jinsi walivyocheza mechi ya kwanza na amewaeleza wachezaji kupambana kushunda mchezo wa leo na kucheza soka safi.

“Mechi ya kesho tunaanza upya, nimewaambia wachezaji wangi kusahau matokeo ya mechi iliyopita na tunaanza upya kabisa, nataka kuona mchezo mzuri na ushindi wa mabao mengi.

Kila mchezaji anatakiwa kupambana kwa sababu kila mtu anayo nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza, Hafiz (Konkoni) ni mzuri na bado anahitaji muda ili kuwa mzuri zaidi,” alisema Gamondi.

Aliongeza kuwa kila mchezaji anatakiwa kuwa tayari ukiangalia safu ya kiungo Pacome Zouzoua na Stephane Aziz Ki wameonyesha kiwango kizuri na kunipa ushawishi mkubwa.

Gamondi alisema kuwa wachezaji wake wako tayari kwa ajili ya mchezo huo na anahitaji kupata matokeo mazuri ambayo watalazimika kusonga mbele na hatimaye kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo hawajawahi kufika kwenye hatua hiyo.

Mwakilishi wa wachezaji wa Yanga, Abdultwalib Mshery alisema wamejipanga vizuri na kocha amewaleza wasahau matokeo waliyoyapata kwenye mechi iliyopita na kuanza upya.

“Kazi iliyobaki kwa sasa ni wachezaji benchi la ufundi limemaliza kazi yake, tunahitaji kupata matokeo mazuri katika mechi yetu ya kesho, tunahitaji kuvuka hatua hii na kucheza makundi ambayo hatujawahi kucheza kwa muda mrefu,” alisema Mshery.

Kuhusu hali yake, alisema yuko fiti na tayari kusaidia timu yake katika kila mechi ikiwemo ya ligi au michuano hiyo ya Kimataifa baada ya kupona majeraha yake ya mguu yaliyomfanya kukaa nje kwa muda mrefu.

SOMA NA HII  HIZI HAPA PONGEZI ZA AHMED ALLY KWA YANGA....