Home Habari za michezo NGOMA ATULIZA ‘PRESHA’ YA ROBERTINHO SIMBA…KANOUTE MHHH…!!!

NGOMA ATULIZA ‘PRESHA’ YA ROBERTINHO SIMBA…KANOUTE MHHH…!!!

Habari za Simba

KOCHA mkuu wa Simba, Mbrazil, Robert Oliveira ‘Robertinho’ amefichua mpaka sasa hana presha yoyote juu ya safu yake ya kiungo kutokana na ubora mkubwa unaonyeshwa na viungo wa kati Mzamiru Yassin na Frabrice Ngoma hali inayopelekea kutapa ugumu wa chaguo la kwanza.

Robertinho ametoa kauli hiyo kutokana na ubora wa viungo hao katika eneo la kati kwa kuweza kuituliza timu na kuweza kutengeneza mashambulizi ambapo mpaka sasa Simba imefanikiwa kushinda mechi nne za mashindano zikiwemo mbili za Ligi Kuu Bara.

Robertinho alisema ubora mkubwa unaonyeshwa na safu yake ya kiungo cha kati kinapelekea kutokuwa na mchezaji mwenye nafasi ya uhakika kutokana na wote kuwa kwenye ubora unaofanana katika kutekeleza majukumu ya timu ndani ya uwanja.

Alisema kila mchezaji amekuwa akionyesha kiwango kizuri kwa kutengeneza muunganiko mkubwa hali iliyopeleka kufanya vizuri na kutengeneza mashambulizi mengi.

“Timu ipo kwenye wakati mzuri kwa ajili ya mashindano ambayo yapo mbele yetu kutokana ukubwa wake, ukiangalia tuna ligi ya mabingway supa ligi, Kombe FA pamoja na michuano ya mapinduzi lakini napata furaha zaidi kwa sababu karibu kila idara wachezaji wamekuwa wakionyesha ubora wa kiwango kikubwa ambacho kinachangia kupata matokeo mazuri.

“Hakuna ambaye anaweza kusema anaweza kuwa na nafasi ya kudumu ndani ya timu yangu kwa sababu wote wamekuwa katika ubora mkubwa, angalia eneo la kati kuna Mzamiru, Ngoma pamoja na Kanuti ambao wote wanaisadia timu kwa kutimiza majukumu yao kwa kila ambaye anayepata nafasi ya kucheza,” alisema Robertinho.

Aliongeza kuwa anawapongeza uongozi wa timu hiyo kwa kufanya usajili mzuri kwa kila mchezaji kuwa na uwino sawa wa kucheza.

SOMA NA HII  TRY AGAIN: SIMBA TUTASAJILI 'VIFAA' KUTOKA ARGENTINA NA URUGUAY