Home Uncategorized FAINALI YA CECAFA LEO,UGANDA V NGORONGORO

FAINALI YA CECAFA LEO,UGANDA V NGORONGORO

 


TIMU ya Taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes leo Desemba 2 itacheza mchezo wa fainali wa Michuano ya Cecafa dhidi ya Uganda.


Ngorongoro Heroes ilitinga hatua ya fainali baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Sudani Kusini.


Inakutana na Uganda ambayo ilishinda mabao 3-1 dhidi ya Kenya mchezo wa hatua ya nusu fainali iliyochezwa Uwanja wa Black Rhino, Academy Karatu.


Fainali hiyo itachezwa Uwanja wa Black Rhino Arusha kabla ya kuchezwa fainali hiyo kutakuwa na mchezo wa play off kumsaka mshindi wa tatu kati ya Kenya na Sufani Kusini.

SOMA NA HII  LIGI YA MABINGWA: PLATEAU UNITED 0-0 SIMBA