Home Uncategorized YANGA YATENGA MILIONI 30 KUPATA SAINI YA MBADALA WA SARPONG

YANGA YATENGA MILIONI 30 KUPATA SAINI YA MBADALA WA SARPONG


 MABOSI wa Yanga inaelezwa wametenga dau la milioni 30 kuipata saini ya mshambuliaji namba moja wa JKT Tanzania, Adam Adam mwenye mabao sita na pasi moja ya bao kati ya 12 yaliyofungwa na timu yake.

Nyota huyo alikuwa wa kwanza kufunga hattrick ya kwanza msimu wa 2020/21 ndani ya Ligi Kuu Bara. Aliwatungua Mwadui FC kwenye ushindi wa mabao 6-1 Uwanja wa Mwadui Complex.


Habari zinaeleza kuwa sababu kubwa ya nyota huyo kuingia rada za Yanga ni kutatua ubutu wa safu ya ushambuliaji ambayo inaongozwa na Michael Sarpong mwenye mabao matatu.

Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze ameweka bayana kwamba ni lazima wafanye mchujo wa washambuliaji wake ambao wanashindwa kufanya vizuri ili kumpata mbadala wake.

“Kiuhalisia matokeo ambayo yanapatikana ndani ya uwanja ni mazuri kwa kuwa tunapata pointi ila kwa upande wa washambuliaji bado haijawa vizuri hivyo ni lazima mchujo ufanyike.

“Nafasi kwenye mechi zetu tunapata nyingi hasa kipindi cha kwanza, kwa mfano kwenye mchezo wetu dhidi ya JKT Tanzania tulipata nafasi tatu ndani ya dakika 45 ila tumefunga moja kuna namna inabidi ifanyike,” amesema.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela kuhusu suala la kumsajili Adam wa JKT Tanzania amesema kwamba bado wanasubiri kuona ripoti ya mwalimu.

“Kuhusu Adam kumsajili ndani ya Yanga kwa sasa mambo bado, tunasubiri ripoti ya mwalimu ili kujua yeye anasemaje,” .
SOMA NA HII  MOHAMED SALAH AFUNGUA AKAUNTI MPYA HUKO ENGLAND