Home Uncategorized POLISI TANZANIA YAMALIZANA NA NYOTA WATATU KWA MPIGO,MMOJA ALIKUWA ANAKIPIGA KMC

POLISI TANZANIA YAMALIZANA NA NYOTA WATATU KWA MPIGO,MMOJA ALIKUWA ANAKIPIGA KMC


 UONGOZI wa Polisi Tanzania, leo Agosti 26 umemalizana na nyota watatu ambao watakuwa ndani ya kikosi hicho kwa msimu wa 2020/21.

Nyota hao ni pamoja na mshambuliaji, Ramadhan Kapera aliyekuwa anakipiga ndani ya KMC yeye amesaini kandarasi ya mwaka mmoja akiwa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake ndani ya wana Kino Boys kumeguka.

 Pia imemalizana na mlinzi wa kulia, Datus Peter ambaye alikua anakipiga ndani ya Klabu ya Mbao FC yeye amesaini mkataba wa miaka miwili akitokea Mbao FC.

Nyota wa tatu ni Kassim Shaban Haruna aliyekuwa anakipiga ndani ya Sahare ya Tanga amesaini dili la miaka miwili.
SOMA NA HII  UNITED YASHINDA VITA YA KUMPATA NYOTA WA NIGERIA MBELE YA SPURS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here