Home Azam FC AZAM FC:DUBE AMEPONA KWA SASA

AZAM FC:DUBE AMEPONA KWA SASA

 


UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa mshambuliaji wao namba moja Prince Dube kwa sasa yupo fiti kwa ajili ya kuendelea kuonyesha uwezo wake ndani ya uwanja baada ya kukaa kwa muda wa wiki sita akitibu jeraha la mkono.

Dube ni namba moja kwa utupiaji ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina aliyechukua mikoba ya Aristica Cioaba.

Aliumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga akiwa kwenye harakati za kuwania mpira baada ya kugongana na beki wa Yanga, Bakari Mwamnyeto.

Amehusika kwenye jumla ya mabao 10 ndani ya Azam FC kati ya 24 ambayo yamefungwa na timu hiyo ambayo ipo nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu Bara na pointi zake kibidoni ni 32.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa Dube yupo tayari kwa ajili ya mechi za ushindani.

“Alikuwa nje kwa muda mrefu ila kwa sasa tayari amesharejea na yupo tayari kwa ajili ya mechi za ushindani na zile za kirafiki.

“Tupo vizuri na maandalizi yanakwenda sawa hivyo ni suala la muda tu kwa mashabiki wa Azam FC kuona uwezo wa nyota Dube pamoja na wengine ndani ya uwanja,” .

SOMA NA HII  AZAM FC YAMTABULISHA JONAS TIBOROHA